| Baadhi ya watu walikula nyama ya samaki aina ya Kasa wakikimbilia Hosptali ya Micheweni |
WATU watatu wamekufa na wengine zaiidi ya 28 wamelazwa katika Hospitali ya wilaya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kula samaki aina ya Kasa mwenye sumu katika shehiya ya Msuka wilayani humo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa Wilaya hiyo,
Dkt. Mkubwa Habibu amesema kwamba tayari wagonjwa waliofika katika
hospitali hiy
o wamelazwa na wanaendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa
madaktari huku akibainisha changamoto ikiwa kukosa ushirikiano pamoja na
taarifa sahihi kutoka kwa waathirika wa tukio hilo.
“Wale wote waliopata kula samaki huyo tunawaomba wafike Hosptal
mapema ili kupata matibabu ya haraka”
alieleza Mganga Mkuu.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya aliyefika
katika hospitali hiyo kuangalia maendeleo ya waathirika hao na kuwataka
wananchi waliotumia samaki huyo kujisalimisha katika kituo cha afya
ili waweze kupatiwa matibabu.
Amina Hamad Omar kutoka kijiji cha Tumbe alisema alipelekewa samaki huyo kutoka msuka kwa ajili ya kitoweo.
"nilipika samaki yule mwenye manofu kama ya nyama ya Ng'ombe baada ya kupika, niliwapatia watoto kabla ya mimi, mara watoto wanalalamika mauimivu ya tumbo" alisema Amina
alisema baada ya hapo waliwachukuwa watoto hao na kuwakimbiliza Hospitali ya Micheweni kwa ajili ya matibabu zaidi.
0 Comments:
Post a Comment