Wananchi Pemba waaaswa kufanya mazoezi


Wananchi kisiwani pemba wameaswa  kujiunga katika vikundi vya mazoezi ili kuimarisha afya zao pamoja na kukuza ushirikiano wa kufanya kazi katika harakati za kijamii.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa kikundi cha mazoezi Gombani fitness club Issa kassim Juma mara baada ya kumaliza kufanya usafi uliofanywana wanakikundi hao katika hospitali ya   vitongoji  cottage chake chake Mkoa wa kusini pemba.

Amesema kupitia vikundi vya mazoezi Afya za wanachi zinaimarika  na kusaidia kupunguza gharama za matibabu lakini kuendeleza kudumisha ushirikiano kwa wananchi wenyewe kwa wenyewe. 

"Ninawashauri wananchi wenzangu wale ambao hamjaingia kwenye hivi vikundi ni kweli vyema  kujiunga ili kuimarisha afya zetu " alisema

 Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi hao Abeid Omar Salum wamesema lengo la kufanya usafi katika hospitali hio ni kuadhimisha mwaka moja wa rais wa zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi na kumsaidia katika kazi za kijamii.

Nae daktari dhamana katika hospitali ya vitongoji cottage Sharif Hamad Khatib amekipongeza kikundi cha mazoezi Gombani fitness club kwa kuamua   kusaidia kufanya usafi katika hospitali ambapo ameviomba vikundi vyengine kuiga mfano wa kikundi hichi kusaidia katika maeneo muhimu. 

Hata hivyo daktari huyo amesema kikundi hicho cha mazoezi ni cha kwanza kujitokeza kufanya usafiri katika hospital hio. 

Aidha amewaasa wananchi kufanya mazoezi kwa kufuata kwa utaratibu wa afya pamoja na kuzingatia aina za vyakula. 

"Nimefarijika sana kuona siku ya leo vikundi vya mazoezi vinakuja kutusaidia kufanya usafi hospitalini hapa na sina Cha kuwalipa lakini  nawashukuru sana  kwa kuonesha  uthubutu huu kwani hichi ni kikundi Cha mwanzo kujitokeza katika my hospitali yetu " alisema 

Awali kabla ya Kufanya usafi  wanakikundi hao walianza kufanya mazoezi ya kukimbia na kuimba nyimbo za hamasa kutoka skuli ya sekondari fidel castro hadi katika hospitali hio..

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment