MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Maendeleo ya
Mtoto (UNISEF), kuifanyia mapitio sera ya Maendeleo ya Mtoto Zanzibar, ili
iweze kwenda sabamba na mweleko wa mahitaji ya serikali yaliyopo sasa.
Othman ameyasema hayo leo Ofisini
kwake Migombani mjini Zanzibar alipozungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika hilo
Bibi Laxmi Bhawani.
Aidha amesema kwamba kutokana na
mambo mbali mbali yanayojitokeza katika utekelezaji wa sera hiyo, hivi
sasa inahitaji kufanyiwa mapitio sambamba na kusaidia mpango wa
kuimarisha liche ya mtoto katika kujenga mustakbali bora wa maendeleo ya mtoto
wa Zanzibar.
Amefahamisha kwamba shirika hilo kwa
muda mrefu limekuwa na mchango mkubwa kuisaidia Zanzibar katika masuala
mbali mbali ya maendeleo ya mtoto hasa wenye mahitaji maalum na lishe
ambapo masuala hayo yamepewa umuhimu mkubwa katika kujenga
maendeleo ya mtoto Zanzibar.
Othman amesema katika majadiliano
hayo pamoja na mambo mengine pia wamekubaliana kushirikiana katika
kustawishi mahitaji mbali mbali ya watoto wenye mahitaji maalum Zanzibar hasa
katika maeneo ambayo yanayonekana kuwa na matatizo zaidi katika ustawi na
maendeleo ya mtoto.
Akizungumzia suala la utunzaji wa
Mazingira, amesema kwamba wamekubalia kutumia mbinu za pamoja za utunzaji
na uhifadhi wa mazingira ikiwemo suala la taka ii yawe na faida kwa maendeleo
ya mtoto na taifa kwa kujmla.
Amesema watoto wenye mahitaji maalum
hasa katika maeneo kama vile ya Micheweni ambayo yanaonekana yapo nyuma
kwa kuwepo matatizo mengi zaidi yanayoathiri maendeleo ya mtoto katika
ukuaji na uimarishaji wa mfumo wa lishe yatapewa kipaumbele.
Hata hivyo, amesema katika jitihada
hizo za pamoja pia mashirikiano yataelekezwa katika utoaji wa elimu zinaohusu
mazingira, maendeleo ya mtoto pamoja na liche bora ili kuwajenga watoto
kukua vyema kimwili na kiakili kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Mwakilishi hyo
makaazi wa Unisef Laxmi Bhawani amesema kwamba Shirika la UNISEF lipo
tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kusaidia
mambo mbali mbali kwa maendeleo ya mtoto na Zanzibar kwa jumla.
Amesesema pia shirika lake
litaimarisha mashirikiano ya wadau na jamii katika kukuuza upatikanaji wa lishe
bora kwa watoto sambamba na kutoa elimu kujenga mwamko wa jamii kwa matumizi
sahihi ya chakula chenye kujenga liche bora kwa watoto.
Amesema kwamba UNISEF
jitiuhada za pamoja kati ya UNISEFU na Zanzibar yatasaidia kujenga uelewa
zaidi kwa jamii na kwamba masuala hayo yamepewa umuhimu wa kipekee katika
kusaidiana na Serikali ya Zanzibar kuwajengea mustakabali bora watoto .
Bibi Laxmi alifika Ofisini
hapo kwa ajili ya mazungumzo rasmi
yaliyohusu ushirikiano kwa masuala mbali mbali na Zanzibar, ikiwemo
maendeleo ya mtoto, lishe pamoja na suala la utunzaji na hifadhi Mazingira ya
Zanzibar.
0 Comments:
Post a Comment