Vijana wa Chakechake Pemba waaswa kuachana na matendo maovu

 


Na Hassan Mselem,Pemba

hmselem@marhabanews.net


Vijana katika Wilaya ya Chake Chake wametakiwa kuachana na vitendo vya uhalifu na udhalilishaji na badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kuzidisha kasi ya maendeleo katika Wilaya hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa mdhamin Wizara ya Habari, Vijana, Utamuduni na Michezo Salum Ubwa Nassor wakati akifungua mashindano ya mpira wa miguu yatakayojumuisha timu 16 za Wilaya hiyo, amesema ripoti mbali mbali zinaonesha kukithiri kwa vitendo vya uhalifu na udhalilishaji visiwani Zanzibar, hivyo basi amesema kuanzishwa kwa Mashindano hayo yatawasaidia vijana kujitambua na kuachana na vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2021 ibara ya 188 inahimiza umuhimu wa michezo na sanaa, hivyo basi amewaomba vijana kulitilia mkazo suala la michezo ili kuhakikisha wanakuwa na afya bora na imara.

Akisoma risala katika ufunguzi wa mashindano hayo mkuu wa jeshi la polisi Wilaya ya Chake Chake Akama Mohammed Shaaban amesema lengo la kuanzishwa kwa mashindano hayo ni kupambana na vitendo vya uhalifu katika Wilaya hiyo kupitia mradi wa polisi jamii wa vijana na michezo.

Mashindano hayo yamejumuisha timu 16 za mpira wa miguu katika Wilaya ya Chake Chake yameanza rasmi Octoba 4\2021 ambapo timu ya Shamasi Fc na Chanjamjawiri Fc zilifungua Dimba ambapo timu ya Shamasi Fc iliilaza bao 1 timu ya Chanjamjawiri Fc bao lililofungwa na Hamad Ali Hamad dakika ya 50, kauli mbiu katika mashindano hayo isemayo ‘’Chake         Chake bila ya vitendo vya uhalifu inawekana’’.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment