
Na Haji Nassor,Pemba
UONGOZI wa Umoja wa akinama wa CCM Tanzania ‘UWT’ wilaya ya Mkoani Pemba, umesema umeridhishwa na kazi ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025, inayofanywa na Mwakilishi wa Jimbo la Chambani.
Ulisema, Mwakilishi huyo amekuwa hatulii kwenye ofisi yake na amekuwa mstari wa mbele, kutekeleza Ilani hiyo, kama alivyoitangaaza wakati akiomba nafasi hiyo.
Akizungumza hivi karibuni, Diwani wa viti maalum UWT wilayani humo, Hassina Sharif Mohamed, alisema kazi kutekeleza ahadi inayofanywa Mwakilishi huyo, wanaridhishwa nayo.
Diwani huyo alieleza kuwa, yapo mambo kadhaa yakiwemo aliyoshirikiana na Mbunge, madiwani na mengine aliyatekeleza bila ya kusubiri fedha za mfuko wa jimbo.
Alifahamisha kuwa, Mwakilishi huyo amekuwa akiendelea kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Chambani wanaondokana na changamoto kadhaa.
“Sisi UWT wilaya ya Mkoani, tunakushukuru na tunakupongeza kwa kazi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, na hivi ndivyo ambavyo tunawataka na wengine kuiga mfano wako,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, Diwani huyo, alisema kilichobakia kwa sasa ni kuhakikisha wananchi kuweka kando tofauti zao, na kushirikiana na viongozi wao wa wadi na jimbo la Chamabni ili kutekeleza vyema.
Aidha Diwani huyo, aliwata viongozi wa matawi ya CCM ya Kwazani Wambaa na Mgagadu waliokabidhiwa madirisha na milango, kuhakikisha wanayafanyia kazi haraka.
“Nguvu ya chama kwanza ni wanachama wenyewe, lakini uwepo wa majengo ya kisasa ya chama, ni hatu nyingine, hivyo kazi iliyofanywa na Mwakilishi ya kuwapatia vifaa hivyo, izae ari ya kuimarisha chama,’’alisisitiza.
Katibu wa CCM tawi la Mgagadu Adam Mussa Kombo, aliahidi kuwa vifaa walivyokabidhiwa wanavitumia kama ilivyokusudiwa.
Kwa upande wake mwanachama wa CCM wa tawi hilo, Tatu Suleiman Juma aliwataka viongozi wengine wa chama na serikali, kuendelea kuwasaidia ili kuendelea kuimarisha chama.
Nae Kaimu Mwenyekiti wa tawi la CCM la Kwazani Wambaa Mohamed Abdalla Haji na Katibu wake Mohamed Khamis Juma, walisema kupatikana na kwa milango na madirisha hayo, ni kupata utulivu wa kuendesha shughuli zao.
Mapema Mwakilishi huyo wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo, alisema ataendelea kutekeleza ahadi zake hatua kwa hatua, hata kama fedha za jimbo wakati mwengine zitachelewe.
Hivyo, amewaomba wananchi na viongozi wa vyama vyote, kumpa kila aina ya ushirikiano, ili kuona anawatumikia vyema, katika kipindi chake cha uongozi.
Mwakilishi huyo kwenye kipindi chake cha awamu ya miaka mitano ya kwanza, aliyajenga matawi saba ya CCM ya jimbo hilo, likiwemo la Chumbageni, Kwanzani, Ngwachani, Chambani, Chumbageni na Pujini.
Mwisho
0 Comments:
Post a Comment