Na - Amina Ahmed
aahmed@marhabanews.net
Pemba
Jumla ya Mikataba 541 kisiwani Pemba iliyokusanywa na kampuni ya Master life kwa upande wa Kisiwani Pemba inatarajiwa kufanyiwa uhakiki kwa lengo la kusaidia kupata fedha na stahiki zao kwa wananchi wote walikuwemo katika kampuni hiyo baada ya serikali kusitisha kuendele kutoa huduma kwa kampuni hiyo .
Akizungumza katika ukumbi wa wa Mesi ya Polisi Madungu Chake Chake Pemba Mkurugenzi Fedha, Mipango Sera na Utafiti na utafiti kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Saum khatib Haji amesema lengo la zoezi hilo limeanza na wananchi wameitikia vizuri wito huo wa kufanya uhakiki baada ya Serikalii ya Mapinduzi Zanzibar kutoa agizo la kufanyika kwa uhakiki huo
Nae Meneja wa kampuni hiyo tawi la Pemba Muhammed Abdalla Salum amesema itaendelea kusimamia zoezi hilo litahakikisha kunapatikana takwim sahihi ambazo zitasaidia kupata stahiki zao kwa kila mwananchi aliekuwa katika kampuni hiyo anapata haki zake kwa mujibu wa sheria.
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uhakiki huo akiwemo Halima Juma Khamis Na Seif Abass Ali wamesema matarajio yao ni kuona wanapata haki zao ambazo waliwekeza katika kampuni hiyo.
Master life ni kampuni inafanya biashara ya fedha inachukuwa fedha na kupokea kutoka kwa wananchi na kurejesha faida kinyume na taratibu ya biashara hiyo ambapo zoezi hilo kwa hapa kisiwani pemba linatarajiwa kumaliza kesho tarehe saba kwa upande wa kisiwani pemba na serikali ya mapinduzi Zanzibar ilisitisha shughuli zake na mahkama kutoa uamuzi juu ya kampuni hiyo.

0 Comments:
Post a Comment