Na Amina Ahmed
aahmed@marhabanews.net
Wizara ya Habari Vijana Sanaa na Michezo imesema itaendelea kuwapa mafunzo ya Uongozi Viongozi wa mabaraza ya Vijana ili kusimamia utendaji katika Shehia zao kwa lengo la kuchangua maendeleo kwenye jamii zao.
Afisa Mdhamini wizara ya Habari Vijana Sanaa na Michezo Pemba Salum Ubwa Nassor ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa viongozi mbali mbali wa mabaraza ya Vijana yaliyofanyika Gombani Kisiwani Pemba.
Alisema ipo haja kwa maafisa wa Vijana kuwapa mafunzo ya Uongozi ambayo yataweza kusaidia kuiongoza jamii ili kusaidia kuleta maendeleo katika jamii sambamba na Tifa kwa ujumla.
Aidha Mdhamini huyo aliwataka Vijana hao kuwa na mashirikiano kuacha mifarakano isiyo ya lazima ambayo itaweza kurudisha nyuma maendeleo ya mabaraza na vijana katika shehia zao
Baadhi ya Washiriki katika mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yataweza kuwasadia kwa kiasi kikubwa katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yao kwenye shehia zao.
Mafunzo hayo ya Siku moja ya Uongozi kwa mabaraza ya Vijana yamewashirikisha Viongozi wakuu wa mabaraza ya vijana ya shehia kusini na kaskazini Pemba.
Imehaririwa na Muhammed Khamis
mkhamis@marhabaews.net

0 Comments:
Post a Comment