![]() |
| Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdallah akifungua Rasmi Mradi wa Ujenzi wa Bweni la wanafunzi wavulana wa skuli ya Sekondari Mafisa akiwa ziarani katika Mkoa wa Tanga. |
Tanzania itandelea
kupiga hatua na kuimarisha ustawi na maendeleo ya wananchi wake kupitia
serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suhulu Hassan.
Mjumbe wa Kamati kuu
ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa ambae pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga, Hemed
Suleiman Abdulla alieleza hayo akiwa katika ziara maalum ya kuimarisha chama
wakati akisalimiana na wanachama na wananchi wa Shina Nambari Tano
Kata ya Kibirashi Wilaya ya Kilindi.
Hemed aliwaeleza
wananchi hao kuwa kuna kila sababu ya kumuunga mkono Rais Samia kwa kudumisha
Amani na Utulivu kutokana na Dhamira ya dhati aliyonayo Kiongozi huyo katika
kuwatumikia wananchi wake.
Alisema kuwa, serikali
ya awamu ya sita inayotekeleza Ilani ya CCM itaijenga Barabara
ilioanzia Handeni kupitia Kilindi na kumalizia Songe kwa kiwango cha lami ili
kurahisha mawasiliano na kuinua hali ya uchumi kwa wakaazi wa wilaya hiyo.
Mjumbe huyo wa Kamati
Kuu alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wa Wilaya ya Kilindi
kujitokeza kwa wingi kushiriki zaoezi la sensa ya watu na
makaazi muda utakapowadia.
Alisema kushirikia
katika zoezi hilo kutaisadia serikali kuweza kupanga mikakati ya maendeleo
kwa wananchi wake sambamba na kupata takwimu sahihi itakayosaidia
kutatua changamoto mbali mbali zinazolikabili taifa kupitia sekta ya Afya, Elim
na sekta nyengine za kijamii.
Akizungumzia suala la
maradhi ya UVIKO-19 Mjumbe huyo wa kamati kuu aliwakumbusha wanachi kujitokeza
kwa wingi kupata chanjo ambayo inatolewa bure na serikali kwa lengo la
kupambana na maradhi hayo hatarishi.
Nao Viongozi wa Jimbo
hilo la Kilindi Mbunge Mhe. OMAR KIGUA na Diwani Mhe. Abubakari walisema Pamoja
na mikakati mizuri iliopangwa na serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wa
jimbo hilo ikiwemo kutengwa kwa Shillingi Millioni Mia Tano wamemuomba Mlezi wa
Mkoa huo kutoa msukumo maalum kwa ajili ya kufanikisha lengo hilo.
Akisoma risala Katibu
wa shina Nambari Tano kata ya Kibirashi Pili Juma Magambilwa alimuomba Mjumbe
huyo wa kamati kuu na Mlezi wa Mkoa wa Tanga kuzipatia ufumbuzi changamoto
zinazowakabili wanachama na wakaazi wa eneo hilo ikiwemo kupatiwa Tawi Pamoja
na kuifanya Zahati yao kuwa Kituo cha Afya ili iweze kutoa huduma kwa wagonjwa.
Akiendelea na ziara
yake katika Wilaya Hiyo, Hemed alifika katika Skuli ya Sekondari Mafisa na
kuweka Jiwe la Msingi Bweni la wanafunzi wanaume wa kidato cha Tano na Sita.
Akilikagua Bweni hilo
Makamu wa Pili wa Rais alionesha kuridhishwa kwake na matumizi ya fedha
zilizotumika kwa ajili ya ujenzi huo ambalo linawanufaisha wanafunzi wapatao
Themanini (80).
Akitoa Shukrani kwa
niaba ya wananfunzi wa skuli hiyo Joice Msengelwa Pius alisema wanafunzi wa
skuli hiyo wanaipongeza Serikali kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo hali
iliyopelekea kupatikana kwa huduma za msingi katika skuli hiyo.
Katika Kuunga Nguvu
jitihada za Wazazi na wananchi wa Mafisa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alihamasisha
mchango maalum kwa ajili ya kumalizia Bweni jengine la kulala wanafunzi ambalo
ujenzi wake umegharamiwa na wananchi wenyewe.
Wakati wa Mchana
Mjumbe huyo wa Kamati kuu alipata fursa ya kuzungumza na Viongozi wa Wilaya ya
Kilindi Pamoja na wanachama kupitia Mkutano wa ndani katika Ukumbi wa Mikutano
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.
Katika hotuba yake
Mhe. Hemed aliwakumbusha viongozi hao kufuata Katiba,taratibu na kanuni za
chama kwa kuachana na tabia ya kutengeneza makundi mapema kabla ya
wakati kufuatia uchaguzi wa Chama unaotarajiwa kufanyika 2022.


0 Comments:
Post a Comment