
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, amesema kwamba maeneo kadha ya visiwa vya Zanzibar yamekabiliwa na changamoto ya kimazingira kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea.
Mhe. Makamu ameyasema hayo leo huko ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, alipozungumza na Ujumbe wa Shirika la Afrika Kusini la CITY CON Africa, linaloshughulikia masuala ya Mipango miji na Utunzaji wa mazingira.
Ujumbe huo ulikutana na Makamu wa rais wa Zanzibar kubadilishana mawazo na kuwasilisha wazo la kuanzisha mradi wa ufukiaji ardhi katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar ili yaweze kutumika kwa shughuli za uwekezaji miradi ya kiuchumi, uhifadhi wa mazingira na kusaidia kuongeza mapato na kukuza maendeleo ya nchi.
Makamu amefahamisha kwamba, kutokana na changamoto ya suala la mabadiliko ya tabia nchi, Zanzibar imetayarisha mpango Mkuu na sera ya kulinda Mazingira kulinda ili kunusuru Zanzibar na janga linalotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mhe. Makamu amekaribisha wazo la shirika hilo la kuanzisha Mradi wa ufukiaji wa ardhi utakaozingatia matumizi sahihi ya aridhi na kuepuka changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na pia kasi kubwa ya ongezeko la idadi watu , na uharibifu wa mazingira linalochagiwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimaizi wa Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, amesema kwamba tafiti mbali mbali zilizofanywa zimebaini Zanzibar kuwepo maeneo mbali mbali yaliyoathiwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema kwamba athari hizo zipo katika sekta mbali mbali zikiwemo kilimo, uvuvi na pia kuharibika mfumo na mtiriritiko wa miongo na upatikanaji wa mvua, bahari kuja juu zaidi na hivyo kuchangia kupunguza kasi na juhudi za kiuchumi nchini.
Mapema Mwakilishi wa Kampuni hiyo Simbarashe Manwere, alimueleza mh. Makamu kwamba Shirika la City Con Afrika lipo tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wadau wengine kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuanzisha mradi mkubwa wa ufikiaji ardhi Zanzibar ili itumike katika shughuli za uwekezaji na kuongeza mapato na kuchangia kukuza uchumi wa Zanzibar.
Zanzibar kama yalivyo maeneo mengine mbali mbali dunaini yaliyozungukwa na bahari adhi yake imekuwa ikipungua kwa kumezwa na bahari hasa kwenye fukwe kutokana na changamoto ya mabadiliko makubwa ya Taibia nchi kunakochangiwa na shughuli za kibinaadamu.
0 Comments:
Post a Comment