| Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, akimkaribisha Balozi Mdogo wa Oman aliepo Zanzibar Said Salim Al-sinawiy, alipofika Ofisi ya Mufti Mazizini Mjini Unguja kujitambulisha . |
| Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akimkaguza baadhi ya vitengo vilivyomo ndani ya Ofisi ya Mufti wakati alipofika kujitambulisha. |
| Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman aliepo Zanzibar Said Salim Al-sinawiy alipofika Ofisini kwake Mazizini Mjini Unguja kujitambulisha. |
| Balozi mdogo wa Oman aliepo Zanzibar Said Salim Al-sinawiy akiagana na watendaji wa Ofisi ya Mufti mara baada ya kufika Ofisini hapo na Kujitambulisha . |
Na Ali Issa -
Maelezo
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia kupata msaada wa kifaa cha kuangalia Mwezi mwandamo kutoka Serikali ya Oman.
Kifaa hicho
kinatarajiwa kufika mwaka huu kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hayo yamesemwa leo
huko Ofisi ya Mufti wa Zanzibar na Balozi Mdogo wa Oman, Said Salum Al-sinawi
alipofika ofisini hapo kujitambulisha kufuatia Balozi aliokuwepo awali kumaliza
mda wake.
Amesema Zanzibar na
serikali ya Omani ni watu wenye udugu wa damu kwa mda mrefu, hivyo ipo haja ya
kuisaidia katika kila nyanja ya maendeleo.
“Mimi naelewa kuwa
Zanzibar na Oman ni ndugu wa damu tutakuwa pamoja ili kuendeleza udugu wetu”
alisema Balozi huyo.
Amesema anacho
kifanya hivi sasa ni kuangalia maombi yote yaliyofika mezani katika ubalozi huo
ambayo yamepangwa kutekelezwa na Balozi aliepita na kuyapa umuhimu na kuyafanikisha kwani hilo ndio jukumu
lake .
“Nimeona maombi
yenu mara tu kufika Ofisini ni jambo jema nitashughulikia hilo ni masuala
muhimu kuweza kutekeleza”, aliongeza kusema balozi huyo.
Amesema ameyaona
maombi yao yapo mezani ikiwemo maombi ya uendelezaji wa ujenzi wa Ofisi ya
mufti,kifaa chakuangalizia mwezi na mambo mengine mengi ambayo ni muhimu.
”Nimeona maombi na
nitayafanyia kazi na hichi kifaa chakuangalizia mwezi kitafika kabla ya Mwezi
mtukufu wa Ramadhani”,alisema Balozi Ali Salum.
Nae Mufti wa
Zanzibar sheikh Saleh Omar Kabi, alimshukuru kiongozi huyo kwa ujio wake kufika
ofisini hapo na kusema ujio huo ni kuendeleza udugu wao wa damu ambao Zanzibar
inafaidika sana na Misaada ya Serikali ya Omani ikiwemi ujenzi wa
Misikiti,nyumba za kihistoria,vyuo na maeneo mengine ya kijamii.
Mufti huyo alisema,
Omani iendelee kuisaidia Zanzibar na isiishie hapo kwani misaada yao imekua ni
chachu ya kuendeleza masuala ya dini ya kislamu katika visiwa vya Zanzibar
hivyo ni muhimu sana kuona dini ya kislamu inasimamiwa misingi yake.
Aidha mufti huo alisema
kuwa wao wako tayari kuendelea na kuisimamia ofisi hiyo kwa nia safi ili
kuendeleza uislamu na kusimamia taratibu zake.
0 Comments:
Post a Comment