Mwakilishi Tunguu akabidhi gari kukuza elimu mkoa wa kusini Unguja

 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Simai Mohammed Said akionekana na Fuaraha baada ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Gari yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kufuatilia masuala ya Elimu ndani ya Mkoa huo.



Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe  Simai Mohammed Said  amekabidhi gari pamoja na mafuta lita 2000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema amekabidhi Gari hiyo  kwa lengo la kusaidia maafisa wa Elimu wa Mkoa huo kufuatilia masuala ya Elimu ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa watoto.

Akizungumza baada ya kukabidhi gari hiyo, Mhe Simai amesema ili waweze kuondokana na kuwa na ufaulu mbovu kwa Wanafunzi wa Mkoa huo, ni lazima uwepo umoja na mashirikiano katika majimbo ya Paje, Chwaka na Uzini.

Aidha amewaomba wawakilishi wa majimbo hayo kuchangia kwa nguvu zote katika masuala ya Elimu, ili kuweza kuinua ufaulu kwa Wanafunzi wao na kuwa mfano mzuri katika Elimu.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini  Unguja Mhe, Rashid Hadid Rashid amempogeza Mhe Simai kwa kuona umuhimu wa Elimu katika Mkoa huo na hivyo  kuamua kuwasaidia Gari watendaji wake kutokana na kuwepo changamoto ya usafiri, ili iweze kusaidia katika ufuatiliaji wa masuala ya elimu.
 
Amesema Mikakati yao katika Mkoa huo ni kuona Elimu inakuwa hivyo ameahidi kuitumia gari hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuitunza ili iweze kudumu na kusaidia katika utendaji wao.

Amewaomba viongozi wa Mkoa huo kuiga mfano kama huo, kwani elimu ni muhimu kwa maisha ya kila siku, na hiyo ni miongoni mwa kuwajali watoto wao.


About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment