| Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akieleeza umuhimu wa vyombo vya habari kuwaunga mkono wanake kushika nafasi za uongozi. |
| Mratib wa mradi wa ushirikishwaji wanawake kushika nafasi za uongozi Salma Amiri Lusangi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani. |
| Mkufunzi wa maswala ya habari Zanzibar Dkt,Abuubakari Rajab akiwasilisha ripoti juu ya uwakilishi wa habari za wanawake katika vyombo mbali mbali. |
| Mwandishi wa habari wa gazeti habari leo upande wa Zanzibar Khatin Suleiman akichangia ripoti hio mara baada ya kuwasilishwa. |
| Mwandishi wa habari kutoka shirikia la magazeti ya Serikali Zanzibaer Mwinyimvua Nzukwi kichangia ripoti hio mara baada ya kuwasilishwa. |
Mkurugenzi wa Chama cha Waaandishi wa habari Wanawake
TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema katika jitihada za kuwaunga mkono wanawake
kushika nafasi mbali mbali za uongozi vyombo vya habari vinawajibu wa kutoa kipao
mbele habari zinazowahusu wanawake viongozi na wale wote ambao wanahitaji
kupaziwa sauti zao kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii.
Dkt,Mzuri aliyasema hayo huko Tunguu Wilaya ya kati Unguja katika ofisi za Chama hicho kufuatia uzinduzi wa ripoti ndogo ambayo inatazama kwanamna gani vyombo vya habri vinawaandika ama kuwaripoti wanawake viongozi katika habari za kila siku visiwani hapa.
Alisema kwa kuwa vyombo vya habari vinanafasi kubwa ya kufanya mabadiliko wakati huu ikiwa ni ikiwemo kuandika na kuripoti matukio mbali mbali yanayofanywa na wanawake viongozi Serikali n ahata wasiokua viongozi ndani ya Serikali.
Alisema vyombo vya habari kupitia mkakati maalumu
wanawake kuwaandaa wanawake kushika
nafasi za uongozi kupitia vipindi vyao vya kila siku kwani wanawake ni watu
wanaoitaji motisha.
Alieleza kuwa kikawaida wanawake wengi wamekua wakishindwa kusika nafasi za uongozi kutokana na kukosa maandalizi bora ya kutaka kushika nafasi hizo badala yake wengi wao huamua kujitokeza kugombea nafasi hizo bila kukosa maandalizi mazuri ya awali.
Akiendelea kufafanua zaidi Mkurugenzi huyo alimtolea mfano Rais Samia Suluhu na kueleza kuwa ni mtu aliepitia hatia hatua mbali mbali hadi kufika kuwa Rais na niwazi kwamba ni miongoni mwa wanawake walioandaliwa na kujitengeneza vyema kushika nafasi tofauti mpaka kuwa Raisi.
Sambamba na hayo alisema ili kutimiza malengo hayo
vyombo vya habari havina budi kujitoa na kutengeneza kampeni maalumu ya kuwainua
wanawake visiwani hapa.
Akiwasilisha ripoti hio mkufunzi wa maswala ya habari
Dkt,Abuubakar Rajab alisema kupitia
utafiti wake wa vyombo mbali mbali vya habari vinavyofanya kazi visiwani hapa
na Tanzania kwa ujumla bado vimekua vikitoa nafasi ndogo sana kwa viongozi
wanawake.
Alisema imekua kawaida kutoona habari ianyomuhusu
mwanamke kupewa kipao mbele kwenye magazeti au ata redio badala yake wengi wao
wanaamini kuwa wanaume ndio wanaopaswa kupewa kipao mbele kila leo.
Akifafanua z kuhusu hali hio alisema wahariri wa
vyombo vya habari hawana budi kuziona changamoto hizo na kuzifanyia kazi
wakijua kuwa kila mtu ana haki sawa na anapaswa kupewa haki yake.
Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hio
Mhariri msaidizi wa shiririka la magazeti ya Serikali Zanzibar Juma Khamis
alisema utafiti huo umewafungua na kuona namna gani wamekua wakishindwa
kuwatendea haki ipasavyo wanawake kupitia vyombo vyao.
Pamoja na hayo alieleza kuwa watahakikisha wanaweka mkakati maalumu kama wahariri kutoa nafasi zaidi kwa wanawake viongozi na wenye nia ya kutaka kuleta mabadiliko katika jamii mbali mbali.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa
ushirikishwaji wanawake katika uongozi kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi
alisema mradi huo wa miaka mine unalenga kuwawezesha wanawake elfu sita kutoka
wilaya 11 za Unguja na Pemba.
Alisema anaamini elimu watakayopatiwa wanufaika wa
mradi huo italeta tija hatimae wanawake wengi wataweza kushika nafasi mbali
mbali za uongozi iwe kwenye jamii zao au hata za kisiasa.
Mradi wa ushirikishwaji wanawake katika nafasi za uongozi unatekelezwa na TAMWA-ZNZ
chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.
0 Comments:
Post a Comment