Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akijibu swali
Namba 36, Septemba 02, 2021 Bungeni jijini Dodoma Septemba 02, 2021 Bungeni
jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali Namba 36 la Mhe. Asia Abdulkarimu Halamga, Mbunge wa
Viti Maalum alilouliza Je, Serikali ina mpango gani wa muda mrefu wa kuwatambua
na kulinda maslahi ya Vijana waliojiajiri katika Sanaa ya burudani kama Video
Vixen na Video King.
Na
Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Serikali
imesema walimbwende, wachezaji, waigizaji, wanamitindo na watu wengine maarufu
ambao hushiriki kwenye Sanaa katika video za wanamuziki kwa lengo la kuiongezea
mvuto kazi husika wanafanya kazi kama watu wengine na wanastahili kusimamiwa
maslahi na haki zao.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline
Gekul Septemba 02, 2021 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali Namba 36
la Mhe. Asia Abdulkarim Halamga, Mbunge wa Viti Maalum alilouliza juu ya mpango
wa kuwatambua na kulinda maslahi ya Vijana waliojiajiri katika Sanaa ya
burudani kama walimbwende.
“Sanaa
hii imekuwa ikihitaji ushiriki wa Video Vixen na Video
Kings, Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria kifungu cha 47(b) mwaka 2019 ili
kuipa COSOTA mamlaka ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mikataba ya kimaslahi kati ya
wenye kazi hiyo ya Sanaa na Vijana wetu wa Video Vixen na Video Kings ili
waweze kupata haki zao za kimkataba” amesema Naibu Waziri Gekul.
Aidha,
Mhe. Gekul ameongeza kuwa watu hao
hushirikishwa na wamiliki wa kazi husika kwa makubaliano maalumu katika kazi
wanazofanya ili kuweza kuifikia na kuivutia hadhira yao.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na. 7 ya mwaka 1999, anaepaswa
kulipwa mrabaha wa kazi ya sanaa ni mtunzi, mbunifu na mtayarishaji wa kazi ya
Sanaa husika.
Pia Mhe. Gekul ametoa rai kwa wadau wote wa
Sanaa ya Burudani kuishirikisha Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ili
maslahi yao yaweze kulindwa kupitia mikataba.
Taasisi
ya COSOTA) ni chombo cha kisheria kilichoanzishwa na Serikali ambayo ipo chini
ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mujibu wa Sehemu ya 46 ya
sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na. 7 ya mwaka 1999 kusimamia sheria hiyo.
0 Comments:
Post a Comment