Na Raya Hamad – OMKR
Maafisa Tehama na wakuu wa vitengo wametakiwa kuwa wabunifu
na kushirikiana katika majukumu yao ya kazi ili kuendana na kasi ya iliyopo ya
ukuwaji wa teknologia ulimwenguni
Mkurugenzi Mipango, sera na utafiti Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Zanzibar Bi Daima Mohammed Mkalimoto ameyasema hayo leo wakati akizindua
mafunzo kwa maofisa tehama na wakuu wa vitengo wa ofisi hio na taasisi
zilizochini yake kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi hio Migombani
Amesema serikali mtandao inatakiwa kuwa hai muda wote
katika kutoa ushirikiano ili iwe ni suluhisho la kiutendaji katika mabadiliko
na kufanya masuala ya tehama kuwa rahisi na kuwa na mfumo mmoja wenye tija kwa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Ndugu Ali Abdi Ali kutoka
Serikali Mtandao amesema maafisa tehama ili waendane kasi ya mabadiliko ya
mawasiliano ni muhimu wawe wanapatiwa mafunzo
ya mara kwa mara jambo ambalo litapelekea kuwa umakini katika utendaji
wao wa kazi
Aidha washiriki wa mafunzo hayo waishukuru Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais na kuomba muendelezo wa mafunzo hayo ili kuwa weledi
zaidi na kufahamu maendeleo ya mawasiliano ya tehama
0 Comments:
Post a Comment