| Miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo wakipitia taarifa za utekelezaji wa mradi huo. |
Wakati muendelezo wa utekelezaji mradi wa VIUNGO
Zanzibar umeingia mwaka wa wapili kamati ya ushauri ya mradi huo inakutana
katika ofisi mradi huo zilizopo mwanakwerekwe
mjini Unguja.
Kamati hio ya ushauri yenye wajumbe 20 ambao ni wakurugenzi kutoka taasisi mbali
mbali za Serikali na binafsi zinazojihusisha iwe kwa namna moja au nyengine na
utekelezwaji wa mradi huo.
Kamati hio ambayo hukutana mara nne kwa mwaka ambapo
kwa mwaka wakwanza wamekutana chini ya mwenyekiti wa mpito Foum Ali Garu na
kufanya vikao vyake vyote vilivotakiwa kwa mujibu wa andiko la mradi huo.
Lengo kuu la kamati hio ni kutoa ushauri kuhakikisha
utekelezaji huo wa mradi unatekelezwa vizuri na kunufaisha walengwa wote
hatimae mabadiliko yaweze kuonekana kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Wakati hayo yakijri katika mkutano huu wa leo wajumbe
hao wamepata Mwenyekiti mpya wa kamati hio ya ushauri ,Mohamed Khamis Rashid
ambae ni Mkurugenzi wa Idara ya kilimo Zanzibar.
Awali mara ya kukabidhiwa nafasi hio Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe hao kuhakikisha wanauelewa vyema mradi huo ili waweze kutoa ushauri wenye tija kwa maslahi ya Taifa.
Akifungua mkutano huo Meneja mkuu wa mradi huo Amina
Ussi Khamis alisema wajumbe wa mkutano huo wanapaswa kuwa huru na kutoa maoni
yao kwani maoni hayo ndio yatakayoongeza ufanisi ikiwemo kukuza na kuendeleza
mradi huo.
Mradi huo wa viungo unatekelezwa na Taaissi ya PDF,kwa
kushirikiana na TAMWA-ZNZ pamoja na CFP Chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya kwa
muda wa miaka mine huku lengo kuu likiwa ni kuwainua wakulima wa Zanzibar
kiuchumi kutoka shehia mbali mbali za Unguja na Pemba.
Muhammed Khamis
Afisa Uhusiano,mradi wa Viungo.
+2557748488800
0 Comments:
Post a Comment