Dkt,Shajak,uwepo wa Sera zinazofanana kati ya Zanzibar na Tanzania ni fursa ya kuongeza ufanisi kwa Z'bar




Raya Hamad Suleiman – OMKR       

 

Katibu kuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt,Omar Dadi Shajak

amesema uwepo wa sera na sheria zinazoendana kati ya Tanzania bara na

Zanzibar ni fursa ya kuongeza ufanisi na kufikia malengo ya taasisi hizo.

 

Ameyasema hayo katika kikao cha mashauriano ya pamoja kati ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza

wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na ujumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu

wenye lengo la kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu hasa katika sekta ya Watu

wenye Ulemavu.

 

Dkt Shajak amesema katika kukuza ufanisi ni vyema kuimarisha uhusiano wa karibu uliokuwepo

wa taasisi zote mbili kuzungumza lugha moja ya kiutendaji kwa vile kila upande una mafanikio

na changamoto za kiutendaji lakini mwisho wa siku tunazungumzia mafanikio na maslahi ya

Watanzania ya Watu wenye Ulemavu.

 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Adam amesema lengo la ujio wao ni

kujifunza kutoka pande zote mbili kwa kubadilishana uzowefu na kuangalia miongozo wapi

panahitaji maboresho pamoja na kupeana mawazo ya kiutendaji.

 

“leo tumejifunza utaratibu mzuri uliopo wa kukusanya takwimu za Watu wenye Ulemavu

ambazo zinakwenda mpaka kwenye Shehia hili tunaondoka nalo na wenzetu wa Zanzibar

tumeona wao bado hawajawa na vyuo katika stadi za kazi na marekebisho kwa Watu wenye

Ulemavu hapa tunaona kuwa tumepata kitu kizuri kwa pande zote mbili na tutafanya kazi kwa

pamoja “alisisitiza Profesa Jamal.

 

Mkurugenzi wa Baraza la taifa la Tatu la Watu wenye Ulemavu ndugu Ussi Khamis Debe

amesema Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na Sekretarieti yake wanashughuli kubwa ya

kuratibu masuala ya Watu wenye Ulemavu kwa Serikali na kijamii kwa ujumla.

 

Nae Mkurugenzi anaeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri

Mkuu ndugu Jacob Mwinula amesifu uwepo wa mfumo wa kielekroniki ambao unarahisisha

kupata taaarifa sahihi kwa ajili ya ustawi wa haki za watu wenye ulemavu, pamoja na suala la

miundo mbinu ambapo amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa hivyo watahakikisha miongozo

hio wanaifanyia kazi kwa manufaa ya kiutendaji.

 

Aidha Jacob amesema Watu wenye Ulemavu wanayo haki na nafasi ya kujiendeleza na kupata

huduma kwa jamii sawa na watu wasio na ulemavu na kuongeza kuwa ushiriki wao katika

maisha ya kila siku ndani ya jamii hauna budi kulenga katika kupunguza au kuondosha maisha

tegemezi

Katika kikao hicho mapendekezo kadhaa yametolewa ya kukuza ushirikiano ikiwemo kuwepo

ushiriki wa pamoja kati ya Zanzibar na Tanzania Bara kwenye ushiriki wa mikutano ya kimataifa

na kikanda.

Kuimarishwa mashirikiano juu ya utekelezaji wa mikataba ya kimataifa juu ya haki za Watu

wenye Ulemavu pamoja na kuangaliwa suala la Watu wenye Ulemavu kama ni suala la haki za

kibinaadamu Tanzania nzima.

Vikao hivyo ni muendelezo wa mikakati ya serikali katika kuimarisha

utendaji kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania

kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa sekta ya Watu wenye Ulemavu.

 


About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment