Na Amina Ahmed,Pemba
aahmed@marhabanews.net
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi amewataka wafanya biashara kutopandisha bei za bidhaa kwani Serikali imefanya punguzo la kodi kwa lengo la kuwanufaisha wananchi na wafanya biashara.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika ghafla ya ufunguzi wa jengo la ZRB Gombani Chake Chake Pemba.
Amesema baadhi ya wafanya biashara wanaitumia vibaya fursa hiyo na kuwazidishia wananchi gharama za matumizi kutokana na kupandisha bei za bidhaa hovyo siku hadi siku jambo ambalo amewataka kuliwacha mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo Dk Mwinyi amebadilisha k utaratibu wa umiliki wa mashamba ya eka ya serikali ambapo awali ilikuwa baada ya kufariki baba na mama hurejeshwa serikalini na kupewa watu wengine na kuagiza sasa watoto wapewe mashamba hayo.
Ziara hiyo katika wilaya ya chake chake Dk Mwniyi amepita katika maeneo mbali mbali ikiwemo barabara ya kipapo mgelema, Hospitali ya Chake Chake ukaguzi wa kisima cha maji chanjaani ambapo katika maeneo yote hayo wananchi walipata kuzungumza na rais huyo na kumweleza kero mbali mbali zinazowakabili na kumuomba awasaidie kuzipatia ufumbuzi.
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi yupo kisiwani pemba atatimiza siku ya tano katika ziara yake ya kikazi ambapo itamalizia katika Wilaya Mkoani kwa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo pia atapokea maoni na kero za wananchi wa wilaya hiyo.
0 Comments:
Post a Comment