Ukosefu uhru wa habari kunaidhofisha jamii.



Shirika la habari la Internews Tanzania, limesema kukosekana kwa uhuru kamili wa kupata na kutoa habari, ni kuidhoofisha jamii katika haki hiyo ya kikatiba.

Hayo yameelezwa na Mkufunzi mwandamizi wa shirika hilo Alakok Mayombo, wakati akiyafunga mafunzo kwa njia ya zoom, juu ya uhuru wa habari, yalioendeshwa na tasisi hiyo kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa Habari Tanzania TAMWA-Zanzibar.

Alieleza kuwa, watoa habari ‘sources’ vinadhani kuwa kukataa kwao kutoa ushirikiano na vyombo vya habari, ni kuwamuzia waandishi wa habari pekee, bali ni kuikosesha jamii habari husika.

“Niwaombe wale wenye mamlaka ya kutoa habari, watoe habari kwa waandishi ili nao watumie vyombo vyao ‘channel’ ili kuwapa habari wananchi juu ya mwelekeo wa serikali yao,’’alieleza.

Hata hivyo, amesema kazi inayofanywa na Internews kwa kushirikiana na wadau wake, inaweza kuwa sehemu ya kupatikana kwa uchechemuzi ambao utawarahisishia wandishi kupata habari.

‘’Zipo sheria kongwe za waandishi wa habari na zipo mpya ambazo haziko rafiki na utekelezaji wa kazi za kila siku kwa waandishi wa habari, ni wajibu kuwa na majukwaa kama haya, ili kuomba kufanyiwa marekesbisho,’’alifafanua.

Akiwasilisha mada ya sheria za habari Zanzibar, mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania MCT ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan, alisema kama maoni ya wadau yaliomo kwenye rasimu ya Habari Zanzibar, kutapatikana sheria bora.

Ali Mbarouk Omar kutoka PPC, Pemba alisema licha ya kuwepo kwa changamoto zinazowakumba waandishi wa habari, bado wana wajibu wa kuuhabarisha umma.

Baadhi ya waandishi waliochangia mada hizo, akiwemo Talib Ussi, Ali Sultan na Rahma Suleiman, walisema bado watoa habari hasa kutoka serikalini, wamekuwa na kigugumizi.

Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA, Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali amesisitiza kuwa, vyombo vya habari ni njia mwafaka katika kukuza uhuru wa kujieleza na kupata habari.

Aidha Dk. Mzuri alisema kuwa, kama vyombo vya habari vitafanya kazi katika mazingira wezeshi na kuwepo kwa sheria imara, itakuwa ni jukwaa bora na imara la kujenga uchumi, demokrasia na uhuru hasa kwa makundi maalum.

“Mkusanyiko huu ni muhimu sana kwetu hivyo ni vyema waandishi wa habari wapaze sauti zao kwa kuleta maslahi na sio kuleta mifarakano,’’alisema.

Akitoa ushuhuda wa changamoto zilizowahi kumkumba katika kazi zake, mwandishi wa habari shirika la Magazeti ya serikali Pemba Haji Nassor Mohamed, alisema mtindo wa kuingilia uhuru wa habari unafanywa na hata na baadhi ya wateule wa rais.

Mkutano huo ni mfululizo wa mikutano kadhaa inayofanywa na shirika la Internews kwa kushirikiana na wadau wao, ili kukuza uwelewa, uweledi kwa waandishi wa habari katika kazi zao za kila siku.
Mwisho.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment