Rais Samia awasili Zanzibar akitokea Malawi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda Lilongwe nchini Malawi. Rais Mstaafu Joyce Banda alifika Lilongwe kuzungumza na   kumpongeza Rais Mhe. Samia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Lilongwe nchini Malawi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mara baada ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment