Mkurugenzi TAMWA-ZNZ atoa wito kwa waandishi kujikita ujenzi wa Demokrasia

Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa




Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA, Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali amesema vyombo va habari vi apaswa kutenda kazi zake kwa lengo la  kujenga uchumi, demokrasia na kutetea makundi muhimu ambayo yako pembezoni.

Kauli hiyo aliitowa wakati alipokuwa akizungumza na wadau na waandishi wa habari katika mkutano kwa njia ya zoom ulioandaliwa na TAMWA-Zanzibar na Internews Tanzania.

Alisema  kuwa kutokana na umuhimu wa vyombo hivyo, mara nyingi makundi mbalimbali yakiwemo ya wanasiasa hujaribu kufanya mbinu nyingi za kuvidhibiti vyombo hivyo.

“Mkusanyiko huu ni muhimu sana kwetu hivyo ni vyema waandishi wa habari wapaze sauti zao kwa kuleta maslahi na sio kuleta mifarakano,’’alisema.

Akitowa mada ya changamoto ya vyombo vya habari mwakilishi kutoka PPC Ali Mbarouk Omar aliwataka waandishi wa habari kupaza sauti zao zitakazotatua migogoro ya jamii na kuifanya kuwa na mshikamano na maamuzi sahihi.

Nae Rashid Omar alisema aliwataka waandishi kuandika habari zao kwa kutumia maadili ya kazi zao, ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Wakitowa ushuhuda wa changamoto zilizowahi kuwakumba katika kazi zao mwandishi Haji Nassor wa gazeti la Zanzibar leo na Rahma Suleiman wa Nipashe waliwataka waandishi wa habari wasirudi nyuma wanapopata vitisho katika kazi zao.

Akichangia mada mwandishi mkongwe Salum Vuai alisema viongozi watakapozidisha ushirikiano na kuacha kuwabana waandishi wataweza kufanya kazi zenye kuleta mafanikio kwa jamii husika.

Watoa mada Ali Mbarouk Omar, Rashid Kombo na Shifaa Said Hassan, wamewaka waandishi hao kutokuwa karibu mno na vyanzo vyao vya habari, kama hali hiyo itatishia kazi yao.

Shifaa alisema, jambo la kwanza kwa waandishi wa habari kuhakikisha habari zao wanazoziripoti zinawasaidia wananchi wa kawaida.

Akifunga mkutano huo, Mkufunzi mwandamizi kutoka shirika la habari la Intarnews Tanzania Alakok Mayombo alisema ipo haja ya kurekebisha baadhi ya sheria za habari kwani zinaonekana kubana uhuru wa habari na utendaji wa kutumikia umma.

Alifahamisha kuwa Tanzania na Visiwani wameridhia mkataba wa haki za binadamu hivyo kuna haja ya sheria hizo kukaa sawa, ili habari ziweze kupatikana kama inavyostahiki.

“Kazi ya uchehemuzi itakapofanywa kwa kiwango husika lengo la kupatikana uhuru wa habari litafanikiwa ,“alisema.
Alieleza kuwa ni jambo lisilopingika kuwa kunyima uhuru wa habari ni kunyima haki za binadamu na kuleta uwajibikaji usiofaa.

“Unapoandika habari kwa wakati itasaidia kutoa maamuzi yatakayoleta maendeleo hivyo linalowezekana leo lisingoje kesho”,alisema.

Mkutano huo uliowashirikisha wadau wa habari na waandishi wa vyombo mbalimbali nchini ni ushirikiano kati ya chama cha waandishi wa habari, Zanzibar Tamwa na shirika la Intanews Tanzania.


 

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment