Na Muhammed khamis
mkhamis@marhabanews.net
Asasi za kirai Nchini Tanzania zimetakiwa kutobaki nyuma na kujikita katika matumizi ya mitandao ya kijamii katika kazi mbali mbali za uchechemuzi kwa maslahi ya Umma.
Kauli hio imetolewa na mkufunzi mwandamizi wa waandishi wa habari kutoka shirika la Internews Tanzania Mama Alakok Mayombo katika mafunzo maalumu kwa njia ya mtandao yaliowashirikisha watendaji mbali mbali wa asasi zisizo za kiserikali Nchini.
Alisema kwa mazingira yaliofikiwa hivi sasa asasi za kirai hazina budi kuwekeza nguvu zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii katika shughuli za uchechemuzi.
Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa utetezi katika mitandao
ya jamii Meneja miradi kutoka shirika la Internews Tanzania Shaban Ramadhan Maganga alisema kuna umuhimu
mkubwa kwa asasi za kirai kuwa wabunifu katika njia za uchechemuzi.
Alisema wakati asasi za kiraia zinafanya uchechemuzi wanapaswa kuwa wabunifu ikiwemo kutumia mmitandao ya kijamii kwani inawafikia wengi kwa njia ya haraka zaidi.
Alieleza kuwa asasi za kiraia zinapaswa kufahamu ili uweze kufanya uchechemuzi uliobora na kufikia malengo unapaswa kujiwekea malengo ikiwemo kulenga makundi maalumu katika jamii.
Akiendelea kufafanua zaidi alisema asasi za kiraia zikitumia vyema taratibu za uchechemuzi ni wazi kuwa watapaza sauti za wasiokua na sauti na hatimae mamlaka husika kuchukua changamoto hizo na kuzifanyika mabadiliko kuleta usawa kwa wote ikiwemo mabadiliko ya kisheria.
Kwa upande wake mkufunzi wa waandishi wa habari kutoka
Internews Tanzania Temigunga Mahondo alisema asasi za kiraia zinapaswa kuandaa
taarifa kwa vyombo vya habari kwa lengo la kusambaza habari zao kwa jamii na
kwa njia ya haraka zaidi.
Alieleza kuwa ili taarifa kwa vyuombo vya habari iweze kupewa kipao mbele kwenye vyombo vya habari inapaswa kukamilika na isoacha maswali kwa wahariri kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuifanya habari yako isiweze kutumika.
Sambamba na hayo mkufunzi huyo alisema ni lazima waandaaji wa taarifa hizo watambue kuwa wahariri wa vyombo vya habari wana kazi nyingi za kufanya hivyo unapowasambazia taarifa yenye mkanganyiko unaweza kujikuta kwa muda mrefu taarifa za taasisi hayo hazipewi kipao mbele ama kutoka kabisa katika vyombo vya habari.
Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo wamesema mafunzo hayo yanapaswa kutolewa pia kwa waandishi wahabari ili kutambua wajibu wao ikiwemo kutodaia posho katika taasisi kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili.
Walisema wanahabari wanapaswa kutambua kuwa wanafanya
kazi kwa maslahi ya jamii hivyo inapotokea wanahari kulazimishwa kupewa fedha
ni kurudisha nyumba jitihada za asasi za kirahi hususani katika kampeni maalumu
ya uchechemuzi.

0 Comments:
Post a Comment