Hospital Mnazi mmoja yakabiliwa na uhaba mkubwa wa gesi kupambana na Corona,40 wafariki Dunia

 

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui alipokua akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupatiwa chanjo ya Uviko 19 katika hospitali ya mnazi mmoja mjini Unguja-Picha na maktaba.

Wakati Dunia ikiendelea kupambana na janga la Uviko 19 ama (Covid 19)visiwani Zanzibar inaelezwa kuwa hospitali kubwa kuliko zote ya mnazi mmoja mjini Unguja inakabiliwa na uhaba mkubwa wa gesi za oksijini huku ikidai kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wa maradhi hayo ambapo hadi sasa tayari watu 40 wameshafariki dunia tangu kuanza kwa wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Taarifa ya hali hio imetolewa na Katibu wa Hospital hiyo Hassan Makame na kueleza kuwa hali si shwari katika hospitali hio na kubainisha kuwa kuna idadi kubwa ya wagojwa na uviko 19 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Alisema katika jitihada za kupamba na hali hio tayari wametuma watu jijini Dar es Salam kupata gesi zaidi ili iweze kwendana na mahitaji husika kulingana na wakati walionao.

Alisema kwa sasa wanahitaji zaidi ya mitungi 300 kwa kila siku tano hivyo wanahitaji mitungi ya hakiba kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa hospitalini hapo.

Akifafanua zaidi katibu huyo alisema kwa sasa wana mitungi 180 ndio inatoyumika idadi ambayo ni ndogo kulingana na mahitaji halisi kwa kipindi hichi ili waweze kuwanusuru wagonjwa wanaohitaji kupumua kwa kutumia gesi.

“Kuna baadhi ya wagonjwa wa corona hawawezi kuishi bila ya kupata oxgen, nawashauri wananchi wachukue tahadhari corona na kufuata miongozo ya watalamu wa afya kwa sababu corona ipo na inaathiri sana”alisema.

Kuhusu mazingira ya matibabu kwa wgonjwa hao alisema wametengewa wodi maalum Hospitalini hapo ili kuepusha maambukizi kwa wagonjwa wengine waliopo hospitalini hapo.

Akizungumzia kuhusu utaratibu wa mazishi kwa wagonjwa wanaofariki na maradhi hayo alisema  kuwa maiti hizo zinakabidhiwa jamaa zao kwa ajili ya mazishi lakini hupewa utaratibu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Waziri wa  afya Nassor Ahmed Mazrui alikiri uwepo wa uhaba wa gesi katika hospitali hio na kueleza kuwa jitihada zaidi zinafanyika kuondoa changamoto hio.

Akifafanua zaidi alisema hadi sasa ndani ya hospital ya mnazi mmoja kuna idadi ya wagonjwa 36 na wengine 40 tayari wameshafariki dunia kwa ugonjwa wa uviko 19.

Katika hatua nyengine alisema  wanatarajia kufungua kambi maalum ya wagonjwa wa corona katika kituo cha afya fuoni kibondeni endapo idadi ya wagonjwa itaongezeka.

Sambamba na hayo Waziri huyo alitoa wito kwa wananchi mbali mbali kujitokeza kuchanja chanjo ya corona kwani hadi sasa hakuna mtu yoyote yule ambae alichanja na kupata ugonjwa huo.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment