Hemed awataka viongozi wa Yanga kuendeleza umoja na mshikamano

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Hmemed Suleiman Abdalla akizungumza na mashabiki na wapenzi wa timu hio katika kilele cha siku ya wananchi uwanja wa Taifa Dar es Salam.

Sehemu ya mashabiki wa timu ya Yanga waliohudhuria uwanja wa Taifa katika kilele cha timu ya wananchi.




Club ya Young African (yanga) leo imetamatisha kilele cha wiki ya Wananchi, kilele ambacho limefanyika  katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar Es Salaam.

Katika kilele hicho Msemaji wa Timu hiyo Ndugu Haji Manara ameweza kuwatambulisha wachezaji watakaochezea timu hiyo, ambao wamesajiliwa kisheria kwa kupeperusha bendera ya  timu hiyo.

Akitoa Salamu zake Mgeni Rasmi katika kilele hicho Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wanachama na wapenzi wa timu hiyo kuzidi kushikamana na kushirkiana ili kuendelea kuikuza timu hiyo.

Amesema ni vyema kwa viongozi wa timu  wakashikamana kwa pamoja kutatua chanagmoto mbali mbali zinazowakabili kwa lengo la kuendeleza uhai wa club hiyo Konngwe nchini Tanzania.

Amesema Serikali zote mbili ile Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan na ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoobgozwa na DK. Hussein Ali Mwinyi  zinaunga mkono jitihada zinazochukuliwa na timu za michezo mbali mbali ambapo viongozi hao  wameahidi kukuza michezo nchini.

Akigusia Suala la Nidhamu Mhe. Hemed amewaasa wanachama  na wachezaji wa timu ya Yanga kudumisha nidhamu wakiwa ndani na nje ya mchezo ili kuijengea heshima timu hiyo na taifa kwa ujumla.

Kilele hicho kimepambwa na shamra shamra mbali mbali ikiwemo tumbuizoi kutoka kwa wasanii akiwemo msanii maarufu kutoka Nchini Congo Kofiolomido.

Club ya Yanga imekuwa washindi wa ligi kuu Tanzania mara Ishirini na Saba (27), Washindi wa Kombe la Tanzania mara nne (04), CECAFA CUP mara tano ambayo katika kuhitimisha kilele hicho imecheza mechi ya kirafiki na Club ya soka ya ZAMACO kutoka nchini Zambia.



About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment