Chanjo ya Corona sasa yazinduliwa rasmi Pemba

 

MRATIBU wa Kitengo cha chanjo Kisiwani Pemba Bakari Hamad Bakari, akizungumza na watendaji mbali mbali wa serikali wakiwemo madaktari kutoka vituo mbali mbali vya afya Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa uzinduzi wa zoezi la uzinduzi wa Chanjo ya Uviko 19, zoezi lililofanyika katika Hospitali ya Chake Chake


MRATIBU wa kitengo cha Chanjo Kisiwani Pemba Dk.Bakari Hamad Bakari akichomwa chanjo ya UVIKO 19 aina ya SINOVAC na Mkuu wa Kitengo cha RCH Chake Chake Asha Ali Abdi, wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo kwa Mkoa wa Kusini Pemba.

AFISA Uwendeshaji Tiba Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Jinsia Wazee na Watoto Pemba Dkt.Yussuf Hamad Iddi, akichomwa chanjo ya Uviko 19 aina ya SINOVAC na mkuu wa kitengo cha RCH chake Chake Asha Ali Abdi, wakati wa uzinduzi wa zoezi la uchomaji wa chanjo Mkoa wa Kusini



Na Abdi Suleiman Pemba

abdisuleiman@marhabanews.

UZINDUZI wa zoezi la uchomaji wa Chanjo ya UVIKO 19 kwa mikoa miwili ya kisiwa cha Pemba, limeanza rasmi kwa watendaji mbali mbali wa serikali wakiwemo watoa huduma za afya.

Uzinduzi huo uliofanyika katika Hospitali ya Chake Chake na kuhudhuriwa na watendaji mbali mbali wa Wizara ya Afya na kuwa wakanza kupata huduma hiyo ya Kuchanjwa wakifuatia na waandishi wa habari.

Akizungumza katika hafla hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Dkt.Mohamed Ali Jape, alisema chanjo ni mpango wa dunia katika kupambana na Uviko 19, baada ya kuthibitishwa na shirika la Afya Duniani WHO.

Aliwataka wananchi kuachana na imani potofu zinazoenea kuhusiana na suala zima la Chanjo, huku madaktari na waandishi wa habari ndio wa kwanza kuchanjwa, kutokana na kazi zao za kuelimisha jamii.

Aidha aliitaka jamii kuitikia wito wa kwenda kuchanjwa chanjo ya Uviko 19, ili kujihakikishaia usalama wao katika wimbi la tatu la Uviko 19 linaloendelea.

“Lazima madartari, watoa huduma katika maeneo ya uwanja wa Ndege, bandarini na watembeza watajii kuchanjwa Uviko 19 kutokana na kutoa huduma kwa jamii”alisema.

Naye Mratib wa kitengo cha chanjo Pemba Dkt.Bakari Hamad Bakari, alisema baada ya kupokea shehena ya kwanza ya Uviko 19, wamelaizikima kuanza kutoa cahanjo kwenye wilaya zote nne za Pemba.

Alisema chonjo hiyo tayari imeshaanza kutolewa Unguja na sasa ni zamu ya Pemba, kwa kushirikiana na viongozi mbali mbali wa serikali.

Alisema katika aina ambayo ipo Zanzibar ni SINOVAC na mtu hutakiwa kuchanjwa mara mbili, kwani ndio chanjo ambayo imekubaliwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kchukua tahadhari kubwa katika kukabiliana na ugonjwa wa Uviko 19, kwani ugonjwa upo na hatari sana.

Mwandishi wa Habari kutoka shirika la Magazezi ya Serikali Zanzibar Ofisi ya Pemba, Bakari Mussa Juma alisema tokea alipochanjwa hakuna mabadiliko yoyote aliyoaona ndani ya mwili wake.

Alisema kinachohitajika ni kujiamini kwa kila mtu, pamoja na kuacha kusikiliza maneno ya baadhi ya wananchi ambao wanaendelea kuwapotosha wenzao juu ya upatikanaji wa chanjo ya Uviko 19.

Kwa upande wake Dk Said Mohamed Ali kutoka maabara ya afya Jamii Wawi, alisema chanjo hiyo imeidhinishwa na WHO, pamoja na Wizara husika na kuwataka wananchi kujitokeza kwenda kupata huduma ya chanjo.

Alisema kwa sasa zaidi ya watu bilioni 5 duniani wameshachanjwa chanjo hiyo, wakiwemo makundi mbali mbali ya watu, wakiwemo wazee wenye umri wa miaka 50.

Naye Zuwena Hassan Ramadhani, aliwataka watendaji wenzake wa afya kuwa watu wa mfano katika kupata huduma ya Chanjo, pamoja na akina mama kujitokea katika zoezi la kuchanja miili yao.


Kwa habari picha na matukio mbali mbali tupigie 0712550666 

Au tutumie email marhabanews01@gmail.com

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment